Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Water and Irrigation Wizara ya Maji 643 2025-06-20

Name

Constantine John Kanyasu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Geita Mjini

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: -

Je, lini mradi wa maji katika Mji wa Geita uliosainiwa Mwaka 2022 utakamilika na kuanza kutoa huduma ikizingatiwa kuwa mradi huu ni wa muda mrefu?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Miji 28 katika Mji wa Geita unaohusisha ujenzi wa dakio katika Ziwa Victoria, ujenzi wa mtambo wa kutibu maji, ulazaji wa bomba umbali wa kilometa 109 pamoja na ujenzi wa matanki matano yenye jumla ya ujazo wa lita 8,900,000. Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 54% ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2025 na kunufaisha zaidi ya wananchi 361,000 wa Mji wa Geita.