Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. CONSTANTINE J. KANYASU aliuliza: - Je, lini mradi wa maji katika Mji wa Geita uliosainiwa Mwaka 2022 utakamilika na kuanza kutoa huduma ikizingatiwa kuwa mradi huu ni wa muda mrefu?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nina swali moja la nyongeza. Mradi wa maji katika Kata ya Maposeni ni muda mrefu sasa tangu maagizo yalipotolewa, tena na Waziri Mkuu. Ni lini sasa Kata ya Maposeni itapata maji?
NAIBU SPIKA: Hiyo Kata iko hapahapa kwa Kanyasu au yako wewe? Mheshimiwa Dkt. Thea kama yako sema ni wilaya gani kwa maana huyu Naibu Waziri hawezi kujua yote hayo. (Kicheko)
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kata ya Maposeni ipo Jimbo la Peramiho, Songea Vijijini.
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, bajeti imeshapitishwa na Wabunge hawa na tutakwenda kutekeleza kuhakikisha kwamba tunamaliza mradi huo, ahsante. (Kicheko)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved