Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Water and Irrigation Wizara ya Maji 644 2025-06-20

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: -

Je, lini kazi ya kuleta maji ya Mto Momba katika Miji ya Tunduma, Mlowo na Vwawa itaanza?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeanza utekelezaji wa Mradi wa Maji Tunduma kwa kutumia maji ya Mto Momba kwa gharama ya shilingi bilioni 119.95 ambao utanufaisha pia Miji ya Vwawa, Mlowo sanjari na vijiji 31 vya Wilaya ya Momba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kazi zinazotekelezwa kupitia mradi huo ni pamoja na ujenzi wa chanzo cha maji katika Mto Momba chenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 21.5, ujenzi wa mtambo wa kutibu maji (treatment plant) wenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 20, ulazaji wa bomba umbali wa kilometa 317, sanjari na ujenzi wa matanki matatu yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 10.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa mradi huo upo kwenye hatua za awali za utekelezaji ambapo muda wake wa utekelezaji ni miezi 18 na kukamilika kwake utanufaisha wananchi 1,245,406 wa maeneo hayo, ahsante.