Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini kazi ya kuleta maji ya Mto Momba katika Miji ya Tunduma, Mlowo na Vwawa itaanza?

Supplementary Question 1

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri na ninampongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha ule mradi wa miji 28 kutoka Same mpaka Korogwe. Watu wa Tanga tunakushukuru sana. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, shida ya maji katika Wilaya za Lushoto, Korogwe Vijijini na Kilindi, bado tatizo lipo. Je, ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba watu wa Kilindi, Lushoto, na Korogwe, wanaendelea kufurahia matunda ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, azma, malengo na makusudio ya Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kwamba inapeleka huduma za jamii kwa wananchi wote Tanzania, mijini na vijijini ili wananchi waondokane na shida hii ya upatikanaji wa majisafi na salama.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwambie Mheshimiwa Mbunge kwamba, maeneo yote ya Lushoto, Kilindi na maeneo mengine, yapo katika ilani, na fedha zimeshaidhinishwa, na maji yatafika huko. Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atapeleka maji huko, ahsante.

Name

Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Vwawa

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO K.n.y. MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza: - Je, lini kazi ya kuleta maji ya Mto Momba katika Miji ya Tunduma, Mlowo na Vwawa itaanza?

Supplementary Question 2

MHE. JAPHET N. HASUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa majibu ya Serikali yanasema kwamba mradi huu utakamilika kwa muda wa miezi 18, je, katika kipindi hicho, maji hayo yatafika kwenye eneo la Vwawa na Mlowo?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa kwamba, maji haya yatakapokamilika ama mradi huu utakapokamilika, Serikali kupitia Wizara ya Maji tutahakikisha kwamba maji haya yanafika kila ambapo wananchi wapo, ama kila ambapo wahitaji wapo, ili maji haya yaweze kuwafikia wananchi. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira, kila patakapokuwa pana uhitaji wa maji haya kwa wananchi, maji yatafika, ahsante.