Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Water and Irrigation Wizara ya Maji 645 2025-06-20

Name

Abdallah Jafari Chaurembo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbagala

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: -

Je, lini maji ya DAWASA yatasambazwa Jimbo la Mbagala Mitaa ya Majimatitu, Machinjioni, Serenge, Changanyikeni, Vikunai, Kongowe na Masaki?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mitaa ya Jimbo la Mbagala inapata huduma ya majisafi na salama isiyo toshelevu kupitia mtambo wa mtoni, sanjari na visima virefu 29 vya maji vilivyopo Mianzini, Nzasa I, Nzasa II, Machinjioni, Kongowe I, Kongowe II, Goroka I, Goroka II na Serenge.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa muda mfupi wa kuboresha huduma ya maji katika jimbo hilo, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026, itafanya usanifu wa mradi wa kutoa maji kutoka Kisarawe II kwa lengo la kunufaisha mitaa ya Kongowe, Vikunai na Changanyikeni.

Mheshimiwa Naibu Spika, mpango wa muda mrefu wa Serikali ni kutumia maji ya Mto Rufiji kwa ajili ya kunufaisha mikoa ya Pwani, Lindi, na Dar es Salaam. Mradi huo upo kwenye hatua ya usanifu ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti, 2025 na kunufaisha mikoa tajwa ikiwemo Jimbo la Mbagala, ahsante.