Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. John Danielson Pallangyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Mashariki

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: - Je, lini maji ya DAWASA yatasambazwa Jimbo la Mbagala Mitaa ya Majimatitu, Machinjioni, Serenge, Changanyikeni, Vikunai, Kongowe na Masaki?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Je, ni lini mradi wa maji wa Kata za Imbaseni, Maji ya Chai, Kikatiti mpaka Maroroni kule Arumeru Mashariki utamalizika?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA K.n.y. WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, tayari tumeshaeleza katika majibu mengi ya msingi ambayo tumeyajibu hapa kwamba bahati nzuri sana bajeti yetu imeshakamilika na Waheshimiwa Wabunge mmepitisha hapa fedha kupitia Wizara hii ya Maji takribani shilingi trilioni 1.06 mmeziidhinisha hapa.

Mheshimiwa Naibu Spika, niwaambie Waheshimiwa Wabunge, wananchi na Watanzania wote, kupitia fedha zile zitakwenda kukamilisha miradi, zitakwenda kufikisha maji, zitakwenda kuondoa changamoto yote ya upatikanaji wa majisafi na salama katika nchi yetu, ahsante.