Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 50 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 646 2025-06-20

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. DKT. JOHN D. PALLANGYO K.n.y. MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Maziwa Kijiji cha Likiushin Mnadani - Arumeru Magharibi?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ina wajibu wa kuhakikisha kuwa inaweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa maziwa kwa kuweka miundombinu muhimu ya ukusanyaji ili kurahisisha upatikanaji wa maziwa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kufanikisha hilo, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2022/2023 ilitenga kiasi cha shilingi bilioni moja kwa ajili ya kujenga vituo 10 vya kukusanyia maziwa ikiwa ni pamoja na Kituo cha Maziwa cha Likiushin, Arumeru Magharibi ambapo kwa sasa ujenzi wa kituo hicho umekamilika kwa 100% na Mkandarasi ameshakabidhi kituo hicho kwa Serikali kwa ajili ya kuanza kufanya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika kukamilisha miundombinu ya utunzaji wa maziwa taratibu za ununuzi na usimikaji wa tenki la kupozea maziwa na generator zinaendelea, ahsante.