Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 51 2026-01-30

Name

Abdulaziz Mohamed Abood

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Mjini

Primary Question

MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:-
Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya
Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa,
Mkundi na Lukobe itakwisha?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA
SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa
Abdul–Aziz Mohamed Abood, Mbunge wa Morogoro Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2025/2026 Serikali
imetenga shilingi milioni 380 kwa ajili ya matengenezo ya
barabara katika Kata za Lukobe na Bigwa, ambapo katika Kata
ya Lukobe, Barabara za Kilombero – Mazimbu Farm kilometa
moja, Tushikamane kilometa moja, Cape Town kilometa 1.6,
Nzimale kilometa moja, na Lukobe kilometa 0.6 zitajengwa kwa
kiwango cha changarawe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, katika mwaka wa fedha
2026/2027 kupitia Miradi ya Benki ya Dunia, Serikali inatarajia
kutekeleza ujenzi wa Barabara ya Kilombero – Mazimbu Farm
kilometa sita kwa kiwango cha zege ambapo kwa sasa taratibu
za kumpata Mhandisi Mshauri zinaendelea kwa ajili ya kufanya
usanifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Kata ya Bigwa, Barabara ya
Vituli kilometa 0.45 itawekwa tabaka la zege kwa shilingi milioni
92.52. Aidha, katika mwaka 2025/2026, Serikali imetenga shilingi
bilioni 1.04 kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi za
Barabara ya Suluhu New City kilometa moja kwa kiwango cha
lami katika Kata ya Mkundi. Utekelezaji wa mradi huu upo hatua
za manunuzi.