Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdulaziz Mohamed Abood
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Mjini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 1
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini ninataka nimwambie, hali ya Barabara za Manispaa ya Morogoro, kata 26 zote ni mbaya mno, zimeathiri uchumi wa Manispaa na barabara zote hazipitiki. Kuna magari yanayokwenda shuleni hayafiki, kuna magari madogo yanayokwenda majumbani mwa watu mitaani hayafiki, wanashusha kwenye main road.
Mheshimiwa Mwenyekiti, taarifa aliyoisoma Mheshimiwa Naibu Waziri ipo kwenye Ilani. Sasa tunataka kujua kama wananchi wa Morogoro, ni lini watatekeleza ahadi hiyo ambapo hali ya kiuchumi katika Manispaa ya Morogoro ni mbaya kutokana na barabara hizo? (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa ambayo ina urefu mkubwa wa barabara ambazo zinahudumiwa na TARURA kwa takribani kilometa zaidi ya 6,400. Serikali imekua ikitenga fedha kwa kadiri zinavyopatikana na kadiri ambavyo Ilani ya Chama chetu cha Mapinduzi imeahidi, na kwa kadiri mipango na bajeti ya Serikali zinavyoelekeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tangu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani amekuta bajeti ya TARURA katika Mkoa wa Morogoro ikiwa na shilingi bilioni 8.7, leo tunavyozungumza bajeti ya TARURA kwenye Mkoa huo ni shilingi bilioni 26.7. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara zilizotajwa tutaendelea kuzitengea fedha kwa kadiri ambavyo mipango yetu ya Serikali inaruhusu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI kumwelekeza Meneja wa TARURA kipindi hiki ambacho tuko kwenye maandalizi ya bajeti, wazingatie vipaumbele vya Mheshimiwa Mbunge, ndugu yangu Abood, na nimpongeze sana kwa ufuatiliaji makini wa Barabara za Manispaa ya Morogoro. (Makofi)
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 2
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mogitu – Balang’dalalu kwa kuwa ni barabara muhimu kwa uimara wa uchumi katika nchi yetu na hasa Jimbo la Hanang? (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaanza ujenzi wa barabara hiyo aliyoitaja Mheshimiwa Mbunge wa Hanang kwa kadiri ambavyo ipo kwenye mipango yetu na Ilani yetu ya uchaguzi. (Makofi)
Name
Joshua Samwel Nassari
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arumeru-Mashariki
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 3
MHE. JOSHUA S. NASSARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona, nina swali moja tu kwa upande wa Serikali. Wilaya kongwe ya Arumeru Makao Makuu yake ni Halmashauri ya Mji Mdogo wa Usa River. Fortunately, kwa miaka yote Halmashauri ya Mji Mdogo ule haina hata kilometa moja ya lami katika Mji wa Usa River. Tulitenga kilometa tano, na wananchi wakafanyiwa sensitization na Wizara kwa ile teknolojia mbadala ambayo imefanyika kwenye maeneo mengine, lakini unfortunately ile ya kwetu ya Meru haikujengwa kilometa tano pale Mji wa Usa River.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali. Ni lini jambo hili litakwenda kutekelezwa ili na yale maandamano ambayo mwaka 2025 kabla sijawa Mbunge yaliyowatoa wananchi wa Usa River kwenda kwa Mkuu wa Mkoa kwa sababu yasifanyike tena? Wananchi walishafanyiwa sensitization na kuachia maeneo yao na hakuna component ya fidia. Ni lini barabara hizi zitatekelezwa (five kilometers) kwenye Mamlaka ya Mji Mdogo wa Usa River? (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nikiri kwamba nimefika kwenye Jimbo la Mheshimiwa Mbunge, tuliambatana naye kwenda kufanya ukaguzi kwenye barabara ambayo tunaijenga kwa kiwango cha lami. Hivyo hivyo, kama ambavyo tumefanya jitihada kwenye barabara ile tuliyoikagua, tutaendelea kufanya jitihada kama Serikali kuhakikisha tunatenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ili wananchi wa Arumeru na Makao Makuu ya Jimbo hilo Usa River waweze kupata huduma nzuri za barabara. (Makofi)
Name
Josephine Joseph Kapoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 4
MHE. JOSEPHINE J. KAPOMA: Je, Wizara ina mkakati gani wa kuja na solution ya kudumu, na hata kama siyo ya kudumu japokuwa ya muda mrefu kwa zile barabara zinazozibwa viraka? Kwa mfano, kuna baadhi ya barabara unakuta zina mashimo, lakini zinazibwa mara kwa mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nilikuwa ninataka kujua kama tunaweza tukapata solution ya kuziba viraka ambavyo vitakaa kwa muda mrefu kwa ajili ya ku-save pesa ambazo zinatumika. (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mbunge wa Mkoa mzima wa Morogoro aliyetoka kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametupa maelekezo sisi TARURA ndani ya Serikali kwa ajili ya kuanza mkakati wa kutumia teknolojia mpya ambayo itajenga barabara zetu kwa gharama nafuu na hivyo tutaweza kuyafikia maeneo mengi na kujenga barabara zinazodumu kwa muda mrefu zaidi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa huu Mkoa wa Morogoro ambao Wabunge wake wameuliza maswali mengi hapa, Mheshimiwa Rais amefanya kazi kubwa sana, tumejenga mtandao wa barabara kwa kiwango cha lami na sasa tumefikisha karibia kilometa 125. Mradi wa TACTIC ambao tulitekeleza kwa awamu ya kwanza tulipeleka zaidi ya shilingi bilioni 19. Mheshimiwa Rais lengo lake ni kutaka kuona anaufungua Mkoa huu mkubwa ambao ni muhimu kwa uchumi ndani ya nchi yetu. (Makofi)
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 5
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa muda. Jimbo la Chemba, Barabara ya kutoka Kwa Mtoro – Sanzawa mpaka Mpendo, barabara hii imekuwa ikipangiwa fedha kila mwaka wa fedha, lakini utekelezaji wake umekuwa ni wa kusuasua.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi tunavyozungumza, barabara hii mawasiliano yake ni ya shida sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Nini mkakati wa haraka na dharura kwa ajili ya kwenda kurejesha mawasiliano ya wananchi hawa ambao wanaendelea kupata adha kila mwaka na Serikali imekuwa ikitenga fedha hii kwa ajili ya kuwahudumia?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimpongeze Mbunge wa Jimbo la Chemba, tangu amehamia Chama cha Mapinduzi, anatekeleza majukumu yake vizuri na kwa kweli hata swali aliloliuliza linazingatia Ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi. Tutampa ushirikiano Mheshimiwa Mbunge katika kuijenga barabara hiyo kadiri fedha zitakavyopatikana. (Makofi)
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 6
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Barabara za Bunda ya kutoka na kwenda Mihingo na ya kutoka Kurusanga kwenda Mikomalilo, karibu barabara tano zote zimeharibika, lakini majibu tunayopata kutoka mkoa na Wilaya, wanasema vibali vya barabara hizo vimesimama mpaka wapate kibali kutoka Makao Makuu ya TARURA. Je, ni lini kibali hicho kitatoka?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali haijasimamisha vibali vya ujenzi wa barabara ambazo tumeshazipitisha kwenye bajeti zetu. Tulichofanya ni tumetangaza zabuni kwa awamu na huo ni utaratibu wa kawaida wa kibajeti. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Getere, Mbunge wa Bunda, tutakamilisha kazi hiyo ya ujenzi kwa kadiri ambavyo tumezitangaza hapo awali.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 7
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Ninaomba kwanza sekunde chache. Majuzi niliomba Mwongozo hapa na kwa kuwa, nimeshawasiliana na Mheshimiwa Waziri wa Madini tumekubaliana mambo yataenda sawasawa. Ninaomba niondoe maombi yangu ya Mwongozo ule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa ninaomba niulize swali dogo. Mheshimiwa Naibu Waziri anasema hawajazuia vibali. Jimbo la Tarime Vijijini Bajeti ya Mwaka 2025/2026 fedha zote za tozo na jimbo, mikataba haijasainiwa hata mmoja. Wamepitia process zote, mikataba haijasainiwa na mvua imenyesha hakuna mawasiliano. Ninaomba Kauli ya Serikali sasa hivi asubuhi hii. (Kicheko)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Jimbo ambao upo kwa kila jimbo tumekuwa tunapeleka fedha kupitia Mfuko wa Matengenezo ambao upo kwenye kila jimbo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, tumekuwa tunapeleka fedha kupitia Mfuko wa Tozo ya Mafuta ambapo, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa maeneo haya ya barabara aliuleta hapa na tukaupitisha na hivyo kuifanya Bajeti ya TARURA nchi nzima ikatoka shilingi bilioni 275 na ikaenda zaidi ya shilingi trilioni moja. Lengo ni kwa ajili ya kuzifikia barabara kama hizi ambazo amezitaja Mheshimiwa Mbunge.
Mheshimiwa Mwenyekiti, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, barabara hizi tunakwenda kuzijenga kwa kadiri ambavyo tumezitengea fedha kwenye bajeti. (Makofi)
Name
Fadhili Sandali Chilombe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduru Kusini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 8
MHE. ENG. FADHILI S. CHILOMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kwenye Jimbo la Tunduru Kusini, ninakotokea, kuna barabara kuu mbili ambazo ni muhimu sana kwa uchumi wa eneo lile. Barabara ya kwanza inaanzia Misechela – Namasakata – Tuwemacho mpaka Mjini; na ya pili inaanzia Mtina – Nasya – Tuwemacho mpaka Mjini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye barabara hizi kila moja ina eneo korofi. Kwa mfano, hii inayoanzia Mtina – Nasya kuna eneo linaitwa Lamitado, pana kipande cha kilomita kama moja hivi ambayo mvua ikinyesha korosho hazipiti pale, magari yanalala pale hata siku tatu, siku nne. The same kwa upande wa Namasakata, kwenye Daraja linaloanzia Namasakata kwenda Chemchem, kuna kipande kina changamoto ambapo korosho ndiyo zinatoka nyingi, lakini huwa tunapata tabu kuzipitisha pale.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kupata Kauli ya Serikali, ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba, maeneo yale yanapata suluhisho la kudumu?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Tunduru Kusini, jana wakati anatoa hoja hapa alitoa elimu kubwa sana ya umeme kwa Mheshimiwa Ado Shaibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara hizi za Tunduru Kusini, maeneo yote korofi sisi tunayafahamu na tunakwenda kuyafanyia kazi. Tumefanya hivyo kwenye maeneo mengi ya nchi yetu kwa kutumia miradi mbalimbali, ukiwemo Mradi wa Agri Connect, pamoja na Mradi wa Rise. Vivyo hivyo, tutaangaza macho kwa ajili ya wananchi wa Tunduru Kusini. (Makofi)
Name
Esther Nicholas Matiko
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 9
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji wa Tarime ni miongoni mwa maeneo ambayo yanapata mvua ya mara kwa mara, na hivyo kusababisha barabara kuharibika na kuathiri shughuli za maendeleo na uchumi za Mji wa Tarime.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka kujua, nini mkakati wa Serikali wa kulingana na mazingira ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ya mvua ya mara kwa mara, kujenga barabara ambazo zitastahamili hali ya hewa ya Mji wa Tarime ili wananchi wa pale waweze kupita muda wote kwenye barabara zao?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya Barabara za Tarime ni kama ilivyo hali ya Barabara za Mji wa Morogoro. Mpango ambao tumeuweka kwenye Mkoa wa Morogoro, vivyo hivyo tutau-extend kwenda Tarime. (Makofi)
Name
Zuberi Yahya Mfaume
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Morogoro Kusini
Primary Question
MHE. ABDUL-AZIZ M. ABOOD aliuliza:- Je, lini kero ya Barabara za Mitaa katika Manispaa ya Morogoro ambazo ni mbovu hususan katika Kata za Bigwa, Mkundi na Lukobe itakwisha?
Supplementary Question 10
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kuniona na kunipa fursa ya kuuliza swali la nyongeza. Jimbo la Morogoro Kusini ni miongoni mwa majimbo ambayo yako katika hali mbaya sana ya miundombinu kwa sababu, sehemu kubwa ya jimbo hili ni milima, na hivyo, inaathiri hata performance yetu katika elimu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia takwimu za ufaulu, tuko chini na hali ya afya tuko hoi. Tuna changamoto ya Barabara ya Dakawa – Bwakila Juu, ambayo kwa kweli haipitiki kabisa. Tuna changamoto ya barabara ya Kolelo – Lukange...
MWENYEKITI: Mheshimiwa uliza swali moja kwa moja.
MHE. ZUBERI Y. MFAUME: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni kwamba, ni kwa kiasi gani tutapewa upendeleo maalumu kutokana na hali mbaya tuliyonayo, kwa ajili ya kuzikarabati barabara hizi?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunalipokea hili, na Serikali, tutalifanyia kazi kwa kadiri ya ambavyo tutapata taarifa za wataalamu wetu tukimshirikisha Mheshimiwa Mbunge. Pia ninampongeza Mheshimiwa Mbunge kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria Ndogo.