Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 52 2026-01-30

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA I. ALEX aliuliza: -

Je, Serikali inachukua hatua zipi kwa Halmashauri ambazo hazitengi fedha za kununua mafuta ya Watu Wenye Ualbino?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji wa mafuta kwa watu wenye ualbino kupitia halmashari zote nchini. Katika mwaka 2024/2025 Serikali ilitenga shilingi bilioni 8.74, kwa ajili ya huduma za ustawi wa jamii na shilingi bilioni 1.4 zilitengwa kwa ajili ya ununuzi wa mafuta maalum ya ngozi kwa watu wenye ualbino.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuzielekeza halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya watu wenye ualbino. Katika mwaka 2025/2026 jumla ya shilingi bilioni 1.9 zimetengwa kwa ajili ya ununuzi wa mafuta ya watu wenye ualbino kwa kuzingatia sera, sheria na miongozo ya utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu.