Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 1 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 1 | 2026-01-27 |
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Mbinga Mjini?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ninamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Jonas William Mbunda.
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa ufadhili wa Benki ya Dunia imeanza utekelezaji wa Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Mbinga Mjini, ambapo sasa Mradi huu upo hatua ya usanifu chini ya Mhandisi Mshauri aitwaye Bosphorus Technical Consulting Corporation ikishirikiana na Building Design Authority Limited pamoja na Masterpiece Consult Limited. Mara baada ya kukamilika usanifu huo ujenzi utaanza mara moja. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved