Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Mbinga Mjini?

Supplementary Question 1

MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Spika, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini pia niishukuru Serikali kwa kuanza mchakato wa kutekeleza Mradi wa TACTIC ambao ndani yake kuna ujenzi wa barabara kilometa 12, lakini pia ujenzi wa soko la kisasa na ujenzi wa stendi. Ninayo maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza; baada ya mchakato huo kuanza ni lini sasa kazi ya usanifu itakuwa imekamilika?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; baada ya usanifu kukamilika ni lini Serikali itaanza kutekeleza hatua nyingine za kuhakikisha kwamba, mradi huo unaanza kutekelezwa? Ahsante.

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Jonas William Mbunda, Mbunge wa Mbinga Mjini.

Mheshimiwa Spika, kazi ya usanifu kwenye Mradi huu wa TACTIC, Awamu ya Tatu, inafanyika kwenye miji 18. Mara tutakapokamilisha kwenye miji yote usanifu huu, kati ya mwezi huu unaoisha na mwezi wa pili, tutaendelea na hatua zinazofuata za kutangaza zabuni ikiwa ni kwa ajili ya kuendelea kumpata mkandarasi mjenzi kwenye maeneo mbalimbali, pamoja na mkandarasi mtaalam mshauri.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Mbinga Mjini?

Supplementary Question 2

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, Halmashauri ya Mji wa Ifakara, Jimbo la Kilombero pia, lina Miradi ya TACTIC ya soko, stendi na barabara za mitaa. Je, ni lini mradi huu utaanza katika Jimbo la Kilombero? Ahsante.

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, Jimbo la Kilombero ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wetu wa TACTIC, Awamu ya Tatu na hivi sasa tuko kwenye kukamilisha usanifu kwenye hii miji yote 19 ya Awamu ya Tatu. Mara tutakapokamilisha usanifu na gharama kubainika mradi utaanza mara moja.

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza kutekeleza Mradi wa TACTIC katika Jimbo la Mbinga Mjini?

Supplementary Question 3

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji wa Bunda, Jimbo la Bunda Mjini ni miongoni mwa miji 18 ambayo na yenyewe inatakiwa itekelezwe Mradi wa TACTIC kwa kujengwa kilometa 25 za lami, stendi ya kisasa, machinjio na soko la kisasa. Ni lini sasa mradi huo utaanza katika Jimbo la Bunda Mjini?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, kama nilivyotangulia kusema, Mji wa Bunda ni miongoni mwa Awamu ya Tatu ya utekelezaji wa Mradi huu wa TACTIC. Mara tu baada ya Serikali kukamilisha usanifu tutakwenda kuanza hatua za ujenzi mara moja.