Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 2 2026-01-27

Name

Jacqueline Ngonyani Msongozi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. NGONYANI aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mshangano - Legele hadi Mletele yenye kilometa 9.2?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, Profesa Shemdoe, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Jacqueline Ngonyani, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha usanifu wa Barabara ya Mshangano - Legele hadi Mletele, kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami ambapo, shilingi bilioni 2.51 zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa awali wa kilometa 5.0 za barabara hiyo. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuweza kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, aidha, wakati tunasubiri upatikanaji wa fedha katika mwaka wa fedha 2025/2026, barabara hiyo imetengewa shilingi milioni 20, kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo ya kawaida. Vilevile, kwenye mwaka wa fedha ujao wa 2026/2027, Serikali imepanga kutenga shilingi milioni 250, kwa ajili matengenezo ya barabara hiyo ili kuhakikisha inapitika muda wote.