Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jacqueline Ngonyani Msongozi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. NGONYANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mshangano - Legele hadi Mletele yenye kilometa 9.2?

Supplementary Question 1

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja dogo la nyongeza, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kabla ya kuuliza swali, ninaomba jina langu lisomeke Jacqueline Ngonyani Msongozi kwa maslahi ya Wanaruvuma.

Mheshimiwa Spika, swali la (a); kwa kuwa, Barabara hii ya Mletele – Mshangano ni muhimu sana kwa ukuaji wa uchumi katika Manispaa ya Songea. Je, Serikali inapochelewesha ujenzi wa barabara hii haioni kwamba, inadumaza uchumi wa Manispaa ya Songea?

Mheshimiwa Spika, swali la (b); Barabara hii ni bypass ambayo inatumika kwa Barabara ya Mtwara Corridor kwa hiyo, kutoka Mletele kwenda Mshangano kwenda Njombe ni barabara muhimu sana, kwa ajili ya kuondoa msongamano wa magari katika barabara kuu hiyo. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba, barabara hii inajengwa kwa haraka ili kuondoa changamoto iliyopo? Ahsante.

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, Serikali haicheleweshi ujenzi wa Barabara hii ya Mshangano - Legele – Mletele, ndiyo maana imekamilisha; imetenga na imeweka fedha ikakamilisha usanifu wa barabara hii. Kinachofuata sasa, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi, ni kwenda kuijenga barabara hii, kwa awali, kilometa tano kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, barabara hii pia, tunatambua kwamba, huwa inatumika kama bypass kwenye barabara kuu ya Songea - Tunduru. Sisi Serikali mwaka ujao wa fedha wa 2026/2027, tutakapotenga milioni 250 barabara hii itakuwa inapitika wakati wote na itaendelea kutimiza jukumu hili la kuwasaidia wananchi kama bypass wakati panapokuwa pamehitajika.

Name

Eng. Johnston Johansen Mutasingwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. JACQUELINE K. NGONYANI aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Mshangano - Legele hadi Mletele yenye kilometa 9.2?

Supplementary Question 2

MHE. ENG. JOHNSTON J. MUTASINGWA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Ninapenda kuuliza swali la nyongeza kuhusu barabara zangu za Jimbo la Bukoba Mjini. Barabara ya kutoka Chemba kwenda Rugambwa, yenye urefu wa kilometa 1.4 na Barabara ya kutoka Kashai kwenda Mngeza, yenye urefu wa kilometa 7.41 zitaanza kujengwa lini kwa kiwango cha lami, kama ilivyoainishwa kwenye IIani ya Chama Cha Mapinduzi? Ahsante.

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, barabara hizi za Bukoba Mjini zitaanza kujengwa kwa kiwango cha lami, kama ambavyo imeainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi, mara tu baada ya Serikali kupata fedha na kutenga, kwa ajili ya shughuli hiyo.