Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 1 | Energy and Minerals | Wizara ya Madini | 9 | 2026-01-27 |
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Mjini
Primary Question
MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: -
Je, lini Kanuni za CSR kwenye migodi zitabadilika ili miradi ya maendeleo isimamiwe na halmashauri kwa mtindo wa Local Fund badala ya mwekezaji?
Name
Dr. Stephen Lemomo Kiruswa Mamasita
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Longido
Answer
NAIBU WAZIRI WA MADINI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Wizara ya Madini ilitunga Kanuni za Wajibu wa Wamiliki la Leseni kwa Jamii (CSR/Corporate Social Responsibility) na kuanza kutumika mwezi Juni, 2023 zikiwa na lengo la kusimamia utekelezaji wa CSR ili kuhakikisha jamii zinazozunguka migodi zinanufaika ipasavyo na uwepo wa migodi husika. Kanuni hizo zimeeleza bayana wajibu pamoja na majukumu ya wadau muhimu wanaohusika na CSR ambao ni mmiliki wa leseni au mgodi na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (halmashauri).
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Miradi ya CSR Kanuni ya 15(1) imeeleza mmiliki wa leseni ya madini atawajibika kutekeleza mpango wa wajibu wake kwa jamii kwa kuzingatia taratibu na ununuzi na anaweza kumwajiri mkandarasi au mtu mwingine yeyote katika utekelezaji wa miradi iliyopo katika mpango. Aidha, Wizara ya Madini imeendelea kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali kwa lengo la kuboresha kanuni za CSR zilizopo.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved