Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 1 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 11 | 2026-01-27 |
Name
Ritta Enespher Kabati
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:-
Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni mara yangu ya kwanza kusimama mbele ya Bunge lako ninaomba kutumia nafasi hii kumshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuniamini na kuniteua kumsaidia kwenye nafasi hii ya Naibu Waziri wa Ujenzi. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, ninakuhakikishia na Waheshimiwa Wabunge hawa kwamba nitatoa ushirikiano kwa 100%. Baada ya kusema hayo ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete ni sehemu ya Barabara ya Ipogolo – Idete yenye urefu wa kilometa 67.47. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii umeanza kwa sehemu ya Ipogolo – Kilolo yenye urefu wa kilometa 33.61 chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia kupitia Programu ya RISE ambapo utekelezaji wake umefikia 98%. Sehemu iliyobaki ya kutoka Kilolo – Idete yenye urefu wa kilometa 33.86, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved