Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza ninaomba kuishukuru Serikali kwa majibu na ujenzi wa barabara ya kilometa 33.6 kutoka Ipogolo – Kibaoni. Ninamwomba Mwenyezi Mungu ambariki sana Mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; changamoto kubwa ya Wilaya ya Kilolo ni barabara zake hazipitiki kabisa kipindi cha mvua. Tuna barabara inayotoka Kilolo – Kising’a – Ukwega – Wotalisoli – Mlafu – Ilula. Hii barabara ni ya kiuchumi mkubwa kabisa lakini haipitiki wakati wa mvua. Je, Serikali ipo tayari sasa kufanya upembuzi yakinifu kwa maeneo korofi tu ili kuweza kujengwa kwa kiwango cha zege ili barabara hizi ziweze kupitika mwaka mzima? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Barabara ya Kitonga ni barabara ya kiuchumi na kimataifa, lakini kuna eneo kama la kilometa 7.6 ambalo linatakiwa kufanyiwa upanuzi. Tunashukuru Serikali imeshatupatia fedha ya kilometa 1.6 na upanuzi unaendelea. Je, Serikali iko tayari sasa kwa kilometa hizi sita iweze kutoa fedha ili lile eneo korofi lote lipanuliwe ili magari yasiendelee kukwama na kupata ajali kubwa katika Mlima Kitonga? Ikiwezekana Mheshimiwa Waziri aje aone adha kubwa ya wananchi inayotokea katika Mlima Kitonga. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara aliyoitaja ya Kilolo – Watalisoli – Ilula kwa sasa Wizara kupitia TANROADS inafanya upembuzi yakinifu kwa barabara yote. Pia, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba mpango wa Wizara sasa hivi, maeneo yote ambayo ni korofi kwenye miinuko na yale ambayo yanakwama, mpango sasa ni kuyadhibiti kwa kujenga ama lami ama zege ili iweze kupitika kwa muda wote. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali lake namba mbili ambalo linahusu Barabara ya Kitonga. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, hii ni barabara ya kitaifa na ndiyo barabara ambayo ninadhani ni kubwa kuliko zote katika nchi hii (T1). Serikali tumeshaanza kufanyia marekebisho eneo la Kitonga ambalo lilikuwa linakwamisha mizigo mingi sana ambayo inaenda DRC na Zambia. Tumeshaanza na tumeshamaliza kilometa 1.7. Katika mwaka huu tunategemea kwamba tunaweza tukaikamilisha yote ili tusiweze kupata changamoto ya magari mengi ambayo yanapita katika barabara hiyo. (Makofi)

Name

Khalid Mussa Nsekela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?

Supplementary Question 2

MHE. KHALID M. NSEKELA: Mheshimiwa Spika, kwanza ninaungana na wenzangu kumtakia heri ya kuzaliwa Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ninaishukuru Serikali kwa kutuletea mkandarasi wa kujenga Barabara ya lami kutoka Kyerwa kwenda Omurushaka, kilometa 50. Hata hivyo, speed yake ni ndogo sana. Je, Serikali ina mkakati na maelekezo gani ya kumsimamia mkandarasi huyu ili amalize barabara hii ili kukidhi kilio cha wananchi wa Kyerwa? Ninakushukuru sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli mkandarasi huyu anakichofanya ni sanifu jenga Barabara ya Kyerwa kwenda Omurushaka. Nimwagize Meneja na Mhandisi Mshauri anayemsimamia ahakikishe kwamba huyu mkandarasi, kwa sababu alikwishalipwa fedha ya awali, aweze kwenda kwa kasi inayotakiwa kulingana na mpango wake wa kazi ambao ameupanga na tumeukubali. (Makofi)

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?

Supplementary Question 3

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninawashukuru. Barabara ya kutoka Omugakorongo – Kituntu – Rwambaizi – Igurwa – Murongo ipo katika Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, imekuwa kwenye manunuzi kwa muda mrefu, ni barabara muhimu kwani inaunganisha nchi yetu na nchi za Afrika Mashariki; na kujengwa kwa kiwango cha lami kutainua uchumi wa Kagera pamoja na Taifa letu. Je, ni lini barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara hii ni kati ya zile barabara zetu kuu, inaunganisha Uganda na Tanzania kupitia Daraja la Murongo. Mheshimiwa Mbunge atakubaliana nami kwamba hii barabara ilikuwa imetangazwa na tulipata mkandarasi, lakini tukashindwana naye kimkataba. Hivyo, hii barabara imetangazwa tena, iko kwenye hatua za manunuzi kuanza kuijenga kwa kiwango cha lami. Tunaanzia Murongo kuja Omugakorongo. Ahsante. (Makofi)

Name

Revocatus Chipando Clayton

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?

Supplementary Question 4

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza.

SPIKA: Mheshimiwa ni swali moja tu.

MHE. CLAYTON R. CHIPANDO: Mheshimiwa Spika, sawa. Ninaomba majibu kutoka kwa Serikali kuhusiana na Barabara ya Kasulu, barabara ambayo itakwenda kuwasaidia wananchi wa Kata za kama Machinjioni, Rubuga, Kagera pamoja na Kata ya Majengo. Barabara iliyopo sasa hivi inawalazimisha wananchi hawa wakitaka kwenda kwenye kata zao lazima wafike mjini halafu warudi nyuma. Ikijengwa Barabara hii ya Kasulu kuanzia pale Msimba kuelekea Ujiji itasaidia wananchi hawa wasiingie mjini wapate shortcut ya kwenda kwenye makazi yao. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge Baba Levo, Mbunge wa Kigoma Mjini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, tuna wakala mbili za barabara, TANROADS na TARURA. Mheshimiwa Mbunge, Barabara tunazozijenga sisi ni kuanzia Ujiji hadi Kigoma Mjini, Mwanga kwenda Mwandiga, pale kwenye Sanamu ya Sokwe kwenda Simbo na Mwandiga. Hizi barabara nyingine tutahakikisha kwamba tunawasiliana na wenzetu wa TARURA ili kuhakikisha hizo barabara zinajengwa na wananchi wasipate changamoto kama alivyozielezea Mheshimiwa Mbunge. Ahsante. (Makofi)

Name

Esther Nicholas Matiko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, upi mpango wa Serikali wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Kibaoni – Dabaga na Dabaga hadi Idete?

Supplementary Question 5

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, Barabara ambayo inaanzia keep left inakwenda mpaka Mogabiri yenye kipande cha takriban kilometa 9.3 iliyopo Tarime Mjini imeharibika sana kiasi cha kupelekea ajali mbaya sana na wakati mwingine vifo. Hata hivyo, kwa sababu tayari mkandarasi yupo na yupo tayari kuanza kazi anasubiri tu malipo ya awali, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kupeleka fedha hizi ambazo ni takriban shilingi bilioni 7.9 ili barabara hii iweze kutengenezwa na kuunganishwa na ile barabara inayoenda mpaka Nyamwaga ambayo tayari imeshakamilika? Ahsante sana.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaomba nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba kipande hicho ni kweli kimeharibika, kilikuwa na lami, lakini barabara ilitangazwa yote. Ilibidi tuanze mbele ili baadaye tuweze kufumua kipande hiki ambacho amekiongelea Mheshimiwa Mbunge. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, tunajua kwamba hatuwezi tukatoka na barabara ya vumbi kutoka Tarime halafu tukaenda kuipata lami mbele. Kwa hiyo, nimhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali tunaandaa malipo ili mkandarasi aweze kulipwa na kuanza kuikarabati, ambayo ni sawa na kuijenga upya hiyo barabara ambayo ina zaidi ya kilometa tisa. (Makofi)