Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 1 | Energy and Minerals | Wizara ya Nishat | 17 | 2026-01-27 |
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza:-
Je, lini fidia kwa wananchi wa Kijiji cha Liugai Kata ya Luilo zitalipwa ili wapishe Mradi wa Umeme?
Name
Deogratius John Ndejembi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chamwino
Answer
WAZIRI WA NISHATI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa nami ndio mara yangu ya kwanza kusimama hapa mbele ya Bunge lako Tukufu tokea kuteuliwa kuwa Waziri wa Nishati, ninaomba nitumie nafasi hii kipekee kabisa kumshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa imani yake kwangu na kuniteua kuweza kumsaidia katika sekta hii ya Nishati na ahadi yangu kwake kwamba sitomwangusha. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, vilevile niahidi Bunge lako Tukufu na Waheshimiwa Wabunge wote kuwapa ushirikiano wa hali ya juu katika utekelezaji wa majukumu yangu. (Makofi)
Mheshimiwa Spika, sasa ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Zacharious Kamonga, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba, 2025 kazi ya uthamini wa fidia kwa wananchi wa Vijiji vya Lifua, Liugai, Masimavalafu katika Wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe imekamilika ikiwa tayari kwa zoezi la uhakiki (verification) pamoja na uwekaji wazi jedwali kwa wafidiwa (disclosure). Aidha, shilingi 6,025,053,947.72 zinatarajiwa kulipwa kwa wananchi 347 waliopisha utekelezaji wa mradi katika Vijiji vya Lifua, Liugai na Masimavalafu na malipo ya fidia kwa wananchi hao yanatarajia kufanyika mwaka wa fedha ujao wa 2026/2027.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved