Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 69 2026-02-02

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza:-

Je, lini Mradi wa TACTIC Awamu ya Tatu utaanza kutekelezwa katika Jimbo la Bunda Mjini?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Ester Amos Bulaya, Mbunge wa Bunda Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi wa TACTIC kwa Halmashauri ya Bunda Mjini utatekeleza miradi mitatu ambayo ni Ujenzi wa Soko Kuu, Ujenzi wa Stendi ya Mabasi na Ujenzi wa Barabara zenye urefu wa kilometa 4.5. Miji yote ya kundi la tatu, ukiwemo Mji wa Bunda, utekelezaji upo hatua ya usanifu. Baada ya hapo taratibu za kutangaza zabuni zitafuata. (Makofi)