Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 5 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 71 2026-02-02

Name

Benjamin Lukubha Ngayiwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kahama Mjini

Primary Question

MHE. BENJAMIN L. NGAYIWA aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuipandisha hadhi Hospitali ya Manispaa ya Kahama kuwa Hospitali ya Rufaa?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kufanya maboresho katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, ikiwa ni pamoja na kuwezesha utolewaji wa huduma za kibingwa. Huduma za kibingwa zinazotolewa ni pamoja na huduma za magonjwa ya ndani (internal medicine), matibabu ya mifupa, magonjwa ya uzazi, magonjwa ya macho, pamoja na huduma za uchunguzi wa mionzi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Kahama Manispaa ina upungufu wa miundombinu muhimu ikiwemo jengo la huduma za dharura, jengo la huduma za wagonjwa mahututi na baadhi ya vifaa vya huduma za uchunguzi. Serikali itaendelea kutenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu muhimu katika hospitali hiyo kisha kufuata Miongozo ya Wizara ya Afya kupandisha hadhi kuwa hospitali ya hadhi ya mkoa.