Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 5 | Good Governance | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 73 | 2026-02-02 |
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza:-
Je, nini hatma ya Mradi wa TASAF nchini?
Name
Regina Ndege Qwaray
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Lulindi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia kukamilika kwa utekelezaji wa Awamu ya Pili ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini, Serikali inaendelea na maandalizi ya Awamu ya Tatu ya Mpango ili kuimarisha hifadhi ya jamii nchini.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuanza kwa Awamu ya Tatu ya Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kunathibitisha dhamira ya dhati ya Serikali ya kuiendeleza TASAF kama chombo cha kimkakati cha utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya 2023, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na Mipango ya Maendeleo ya Muda Mrefu, wa Kati na Mfupi.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika awamu hii mkazo utawekwa zaidi kwenye Kaya kuhitimu, kujitegemea kiuchumi, ajira pamoja na ushirikishwaji wa kaya katika mifumo ya kawaida ya huduma za Serikali. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved