Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 5 Water and Irrigation Wizara ya Maji 77 2026-02-02

Name

Azza Hilal Hamad

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:-

Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Vijiji 18 vya Tinde package?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Azza Hillal Hamad, Mbunge wa Itwangi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na mazungumzo na Serikali ya India ili kupata kibali cha kuendelea kutumia fedha kiasi cha dola za Marekani milioni 6.9 zilizobaki kwenye mkopo nafuu wa dola za Marekani milioni 268.35 kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa Usambazaji katika Miji ya Tinde na Shelui sambamba na vijiji 18 vya Wilaya ya Shinyanga pamoja na Iramba.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa hatua iliyofikiwa na Serikali imeshawasilisha ombi maalum kwa Serikali ya India mwezi Januari, 2026 baada ya kusitishwa kwa matumizi ya mkopo huo. Ni mategemeo ya Serikali kuwa taratibu za kuruhusu matumizi ya fedha hizo yatakamilika na Wakandarasi kupatikana kabla ya kwisha kwa mwaka huu wa fedha 2025/2026.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, katika mpango wa muda mfupi, Wizara itaunda timu ya wataalam ambayo itafanya tathmini katika jimbo la Itwangi ili kubaini na kuwezesha vijiji vyote vilivyo karibu na mitandao ama matoleo ya maji vinasogezewa huduma.