Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Vijiji 18 vya Tinde package?

Supplementary Question 1

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba niishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; je, Serikali ipo tayari sasa kuleta timu ya wataalam mara baada ya Mkutano huu wa Bunge?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Serikali ipo tayari kutumia sasa Mradi wa Bukene pamoja na Mradi wa Isemela ambao bado unatekelezwa kuweza kufikisha huduma ya maji katika Vijiji vya Zobogo, Tinde, Nuru pamoja na Igulamya? Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa Serikali iko tayari na kama nilivyojibu katika swali la msingi, Wizara inatarajia kuunda timu ambayo itaenda kule Itwangi na kwenda kufanya tathmini na kujiridhisha na hali halisi ya huduma ya upatikanaji wa maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika miradi 3,714 ambayo Serikali iligharimu takribani shilingi trilioni 1.8, ndani ya Itwangi kulikuwa na miradi tisa iliyokamilika yenye gharama ya shilingi bilioni 12.7. Ndani ya Jimbo hili tunayo miradi inayoendelea miwili ambayo ina gharama ya shilingi bilioni 8.9 ikiwemo na kuhakikisha kwamba vijiji vilivyobaki katika eneo hilo ni vijiji 14 tu ambavyo vimebaki bila kuwa na huduma ya maji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, eneo la Tinde, pamoja na Didia, pamoja na Samuye yote yataingizwa katika utaratibu wa kupata huduma ya maji safi na salama. Ninakushukuru sana. (Makofi)

Name

Arif Suleiman Premji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Vijiji 18 vya Tinde package?

Supplementary Question 2

MHE. ARIF S. PREMJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Serikali iliahidi kuboresha miundombinu ya maji kwa kuwajengea tenki la lita 1,000,000 Kijiji cha Likonde, Kata ya Mayanga na ahadi hiyo iitolewa tarehe 27 Septemba, 2022 ambalo litaenda kuwasaidia wakazi zaidi ya 24,000. Je, ahadi hiyo itatekelezwa lini? Ninaomba nisisitize neno “lini?”

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, samahani kidogo, ninaomba kujua ni jimbo gani.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, ni jimbo gani tena?

MHE. ARIF S. PREMJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni Jimbo la Mtwara Vijijini.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutekeleza miradi nchini kote na nchi yetu ina vijiji takribani 12,318. Katika utekelezaji wa miradi ni vijiji 1,575 tu ambavyo vimebaki kutofikishiwa huduma rasmi ya maji. Kwa hiyo, nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge, eneo hilo tunalichukua likiwemo ndani ya miradi 878 ambayo haijakamilika yenye gharama ya shilingi trilioni 1.3. Tunaamini kwamba miradi hii itakapokamilika yote kwa ujumla na eneo ambalo Mheshimiwa Mbunge ameliongelea basi litakuwa limekamilika katika utekelezaji huo. (Makofi)

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Vijiji 18 vya Tinde package?

Supplementary Question 3

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri, atakubaliana nami kuwa, kuna miradi miwili Makete ambayo walisaini takribani miaka minne imepita na miradi hii haijaendelea. Mradi wa Usalimwani, Mfumbi, Kidope na Madihani imesimama hadi saizi. Kwa kuzingatia utendaji wako wewe, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Waziri wake wanafanya kazi vizuri sana; Ni ipi lugha ya matumaini kwa wananchi wa Makete ili waweze kupata maji kwenye miradi hii miwili? Ahsante.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Kaka yangu Mheshimiwa Festo Sanga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa tunakiri kwamba kumekuwepo na changamoto katika utekelezaji wa miradi hii miwili, lakini Serikali sasa imeshaweka mkakati maalum wa kuhakikisha kwamba tunaenda kumrejesha mkandarasi ambaye alikuwa ameshaondoka, alikuwa ameshasitisha utekelezaji wa mradi na sasa madai yake tayari Serikali imeyafanyia kazi na atarudi site na ataendelea kufanya kazi ili mradi ukamilike kwa wakati. (Makofi)

Name

Kija Limbu Ntemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katoro

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI K.n.y. MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Vijiji 18 vya Tinde package?

Supplementary Question 4

MHE. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nianze na kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea maji katika Mji wa Katoro akiyatoa eneo moja linaitwa Chankorongo. Tangu dunia iumbwe maji hayajawai kufika Katoro, lakini sasa yamefika Katoro kwa gharama ya shilingi bilioni nane.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninataka kufahamu maji yameshaletwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, je, ni lini sasa Serikali itakuja kusambaza maji hayo ili wananchi waweze kunufaika na maji kuliko kubaki tu na historia ya kwamba maji yamefika Katoro na hayajasambazwa?

Mheshimiwa Naibu Spika, nimwombe pia Mheshimiwa Waziri…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge, swali la nyongeza ni moja.

MHE. KIJA L. NTEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana.

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ntemi Kija, Mbunge wa Katoro, hakika ameanza kazi yake vizuri na anafanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Naibu Spika, kitu cha kwanza tunachohitaji katika utekelezaji wa miradi hii ni kupata ama kubainisha chanzo cha maji na baada ya hapo kujenga miundombinu (transmition line main) na baada ya hapo sasa tunakuja kwenye usambazaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo nimtoe hofu kwa sababu kazi ya kupata chanzo imekamilika, kazi ya kujenga miundombinu ya kufikisha maji katika eneo la Katoro imekamilika. Sasa kazi iliyobaki ni ndogo sana kwa Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, usambazaji wa maji katika Mji wa Katoro unaenda kufanyika kwa haraka sana. (Makofi)