Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 5 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 78 | 2026-02-02 |
Name
Isack Joseph Copriano
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Monduli
Primary Question
MHE. ISACK J. COPRIANO aliuliza:-
Je, lini Serikali itapeleka fedha ili kukamilisha Mradi wa Maji wa Vijiji 13 vya Jimbo la Monduli?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Isack Joseph Copriano, Mbunge wa Jimbo la Monduli, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na awamu ya kwanza ya upanuzi wa Skimu ya Maji ya Jiji la Arusha kutoka eneo la Ngaramtoni kwenda Vijiji 13 vya Nanja, Mti Mmoja, Arkaria, Arkatan, Lepurko, Engāaroj, Losimingori, Lashaine, Meserani Juu, Meserani Bwawani, Engorika, Engiloriti na Naalarami vya Wilaya ya Monduli mkoani Arusha. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 61.5, ujenzi wa tanki moja lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 500,000, ujenzi wa mbauti mbili za kunyweshea mifugo sambamba na ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea maji.
Mheshimiwa Naibu Spika, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 15% ambapo kwa mujibu wa mkataba unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2026 na unatarajiwa kunufaisha zaidi ya wananchi 34,000. Aidha, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha utekelezaji wa mradi huo unakamilika ili uweze kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi na itahakikisha fedha zinapelekwa kadri zinavyopatikana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved