Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 5 | Health and Social Welfare | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 87 | 2026-02-02 |
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-
Je, Serikali imejipangaje kuhakikisha wanawake wajasiriamali wanashiriki moja kwa moja kwenye utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeweka mikakati mbalimbali katika kuhakikisha wanawake wajasiriamali wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 hususani Nguzo ya Kwanza ya Uchumi Imara, Jumuishi na Shindani na Nguzo ya Pili ya Uwezo wa Watu wa Maendeleo ya Jamii.
Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati hiyo ni pamoja na: kupunguza mkwamo na kupanua upatikanaji wa mitaji na masoko kwa wanawake ili kuongeza uzalishaji; kubainisha na kutekeleza jitihada zenye lengo la kuwawezesha wanaume na wanawake kutambua na kutumia fursa za kiuchumi; utekelezaji wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi; na kuwezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali, teknolojia na viwanda ili biashara zao zikue na kuchangia uchumi wa Taifa.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved