Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 88 2026-02-02

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Primary Question

MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Chuo cha VETA Tarafa za Nyabiyonza na Nyakakika kwani kuna umbali mrefu toka Chuo cha VETA Kayanga?

Name

Omari Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako na kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mbunge wa Karagwe, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli katika Wilaya ya Karagwe, Serikali imejenga Chuo cha VETA cha Wilaya kilichopo Kayanga ambacho kina mabweni na kinaendelea kutoa mafunzo. Kwa sasa wanachi wa Tarafa za Nyabiyonza na Nyakakika wanaweza kuendelea kutumia chuo hicho kwa kuwa kinatoa huduma ya malazi katika mabweni yaliyojengwa kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka umbali mrefu.