Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 9 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 137 | 2026-02-06 |
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:-
Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Shule ya Sekondari Sanzate na Tirina - Bunda?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninaomba uridhie kwamba majibu nitakayoyasoma hapa ndiyo yachukuliwe kama majibu rasmi ya Serikali yale yaliyokuwa tumeyatanguliza yana marekebisho kidogo.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitoa Shilingi Milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa manne, jengo la utawala, maktaba, maabara tatu, chumba cha TEHAMA, matundu ya vyoo ishirini na matenki ya kuvuna maji ya mvua, katika shule mpya ya Tirina. Pia, Serikali imetoa Shilingi Milioni 140 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa manne, ofisi moja na matundu nane ya vyoo, ukamilishaji wa madarasa matatu na ofisi moja katika Shule ya Sekondari Sanzate.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027 Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha miundombinu yote iliyobaki kwenye shule hizi mbili za Tirina na Sanzate.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved