Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Shule ya Sekondari Sanzate na Tirina - Bunda?
Supplementary Question 1
MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninauliza tu maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; TAMISEMI ni lini sasa watakuwa na chombo ambacho kinakuwa kinaangalia kwamba miradi mingi wanayopeleka kwenye maeneo ya vijijini, sekondari na maabara na vitu vingine, inamalizika na wakae wanajua kwamba imemalizika kikamilifu? Ni lini watakuwa na hicho chombo cha kutazama sekondari ipi haijamalizika wakamalizia? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali la pili; Shule ya Sekondari ya Sanzate imejengwa na wananchi, tumei-support milioni 140 yakaja hapa maombi, tumeleta maombi maalum ya milioni 420, ilikuwa bajeti ya mwaka juzi, wakasema itatoka haikutoka, mwaka jana haikutoka. Je, ni lini sasa hizo hela zitatoka ili Shule ya Sanzate imalizike? (Makofi)
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO): Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali langu la msingi mwaka wa fedha 2026/2027 tunakwenda kutenga fedha kwa ajili ya kumalizia miundombinu kwenye shule hizi mbili; Shule ya Sanzate pamoja na Shule ya Tirina. Tunatambua kwamba katika Shule ya Tirina miundombinu ambayo haijakamilika ni maabara tatu, maabara ya physics, chemistry na biology, vilevile jengo la TEHAMA ambalo hatujakamilisha kuingiza miundombinu ya umeme, tutakwenda kuikamilisha.
Mheshimiwa Spika, kwenye Shule ile ya Tirina tukishatenga fedha mwaka ujao wa fedha tunakwenda kukamilisha kujenga jengo la Utawala, jengo la TEHAMA, maabara tatu pamoja na maktaba ili kuleta ufanisi wa mazingira mazuri ya kujifunzia kwa watoto hawa ambao Mheshimiwa Mbunge Getere amekuwa akiwapambania sana sana na ninamwahidi tutaambatana naye kwenda Jimboni kwa ajili ya kuwatembelea wananchi hawa. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved