Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 138 2026-02-06

Name

Hamoud Abuu Jumaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibaha Vijijini

Primary Question

MHE. SUBIRA K. MGALU K.n.y. MHE. HAMOUD A. JUMAA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupandisha hadhi Mji Mdogo wa Mlandizi kuwa Mji kamili?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamoud Abuu Jumaa ambalo leo limewasilishwa na Mheshimiwa Subira Khamis Mgalu na nimpongeze kwa kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Halmashauri huanzishwa au kupandishwa hadhi kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na 288 pamoja na mwongozo wa uanzishwaji wa maeneo ya utawala ambao tumeutoa mwaka 2014, ambao umeainisha vigezo na taratibu zinazopaswa kufuatwa ili kuanzisha au kupandisha hadhi Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa mwongozo mchakato wa kuanzisha Halmashauri mpya huanza na kusudio ambalo hupaswa kujadiliwa katika vikao vya ngazi ya Vijiji/Mitaa, Kata, Halmashauri, Wilaya na Mikoa. Kusudio hilo huwasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kupitia Katibu Tawala wa Mkoa husika kwa ajili ya kufanyiwa tathmini na ufuatiliaji ili kuhakikisha ufikiwaji wa vigezo husika.

Mheshimiwa Spika, ninapenda kuielekeza Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha kufanya michakato iliyoainishwa kwenye sheria zetu na mwongozo wa uanzishwaji wa maeneo ya utawala.

Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha. (Makofi)