Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 9 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 139 2026-02-06

Name

Dr. Yahaya Esmail Nawanda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. DKT. YAHYA E. NAWANDA aliuliza:-

Je, lini Barabara za Chikalule hadi Lihanga na Lochinu hadi Mkwiti zitajengwa?

Name

Kwagilwa Reuben Nhamanilo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Handeni Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Yahya Esmail Nawanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutenga bajeti na kujenga barabara katika miinuko mikali kulingana na upatikanaji wa fedha ambapo hadi sasa imeshajenga Barabara ya Miyuyu hadi Hospitali ya Rufaa ya Ndanda yenye urefu wa kilometa 4.5 kwa tabaka la lami kwa gharama ya shilingi bilioni 2.25. Aidha, ujenzi wa kilometa 0.6 kwa kiwango cha zege kwenye eneo la mwinuko mkali katika Barabara ya Namdimba - Chiwata kwa gharama ya Shilingi Milioni 975.98 unaendelea kutekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na ujenzi wa barabara ambazo zipo kwenye maeneo ya milima mikali katika Jimbo la Newala Vijijini, zikiwemo Barabara za Lihanga na Chikalule kilometa 1.5 na Barabara ya Mkwiti - Lochino - Nyangao kilometa 11.1 kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)