Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 9 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 142 | 2026-02-06 |
Name
Mattar Ali Salum
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shaurimoyo
Primary Question
MHE. MATTAR ALI SALUM aliuliza:-
Je, Serikali haioni haja ya kuongeza wigo wa fedha za mazingira ili kusaidia juhudi za Zanzibar kukabiliana na athari hizo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mattar Ali Salum, Mbunge wa Jimbo la Shaurimoyo kama ifuatavyo:
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha zinaongeza wigo wa fedha za mazingira kupitia vyanzo vya mapato ya ndani na nje ili kusaidia juhudi za Zanzibar kukabiliana na athari hizo.
Mheshimiwa Spika, hatua hizo ni pamoja na: kutenga fedha kupitia Bajeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kutafuta fedha kutoka katika Mifuko mbalimbali ya Kimataifa ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi ambayo ni pamoja na Mfuko wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund), Mfuko wa Mazingira wa Dunia (Global Environment Facility) na Mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi (Green Climate Fund) na kuendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kuongeza wigo wa fedha katika eneo la mazingira.
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea kuongeza fedha za Mazingira kadri ya fedha za miradi zitakavyokuwa zinapatikana. Hadi sasa, jumla ya miradi 10 yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 97.6 imetekelezwa na kukamilika kwa pande zote mbili za Muungano. Aidha, Serikali ipo katika maandalizi ya miradi mitatu yenye thamani ya takribani shilingi bilioni 62.6 ambayo ipo kwenye hatua za awali za maandalizi.
Mheshimiwa Spika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved