Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 129 | 2026-04-20 |
Name
Dr. George Venance Lugomela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:-
Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. George Venance Lugomela, Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Senani – Gula ni barabara inayounganisha Kata ya Senani, Mpindo na Kata ya Lalago katika Barabara ya Senani – Zebeya – Lalago katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa yenye urefu wa kilometa 38.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imeanza kufanya ukarabati wa barabara hiyo urefu wa kilometa 12 kwa gharama ya shilingi milioni 125, ambapo kazi hiyo inaendelea na mkandarasi anaendelea na kazi. Kazi nyingine zinazoendelea katika barabara hiyo ni pamoja na kunyanyua tuta meta 320, kujenga makalavati mistari mitatu na kuchimba mitaro kilometa 6.6.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuendelea na ukarabati wa barabara hii, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali imetenga shilingi milioni 200 kwa utekelezaji. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved