Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. George Venance Lugomela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Primary Question
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:- Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa vile barabara hii ilikuwa na changamoto ya kupitika kabla ya mvua za mwaka huu na mvua za mwaka huu zimenyesha kwa wingi na kuiharibu zaidi. Je, ni ipi tathmini mpya ya Serikali ya kuhakikisha kwamba ule uharibifu ambao umetokea mwaka huu unafanyiwa kazi? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, Mheshimiwa Waziri atakuwa tayari kuambatana nami kwenye jimbo ili kujionea hali halisi ya barabara hii, lakini pia na barabara nyingine katika Wilaya ya Jimbo la Maswa Mashariki?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Dkt. George Venance Lugomela, Mbunge wa Maswa Mashariki amefuatilia sana barabara hii Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na sisi tunamhakikishia kwamba tutahakikisha barabara hii inaendelea kujengwa. Tunafahamu kwamba kumekuwa na mvua nyingi na uharibifu umeendelea kutokea, hasa msimu huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na ujenzi ambao umekuwa ukifanyika, tunaendelea kufanya tathmini ya uharibifu mwingine ulioongezeka kwa ajili ya kutenga bajeti kwa ajili ya kwenda kufanya ukarabati huo. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Dkt. Lugomela kwamba, tutafanya tathmini na kazi hiyo inaendelea na taarifa tunaendelea kuzipokea, Ofisi wa Waziri Mkuu, TAMISEMI kwa barabara hiyo, lakini na barabara nyingine zote kote nchini kwa ajili ya kutenga fedha kwa ajili ya matengenezo ya dharura, lakini na matengenezo ya mara kwa mara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, niko tayari kuambatana na Mheshimiwa Dkt. Lugomela kwenda Maswa Mashariki. Tutakaa mimi na wewe Mheshimiwa Mbunge tupange ratiba na tuone lini tutapata fursa twende tukakague barabara hii na barabara nyingine kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunaboresha usafiri na usafirishaji kwa wananchi. ahsante sana.
Name
Fagason Aron Nkingwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:- Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?
Supplementary Question 2
MHE. FAGASON A. NKINGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa kuwa barabara zimekuwa zikiharibika nchi nzima, lakini ninayo barabara inayotoka Lulembela – Kiseke ambayo imekuwa ni hatari sana kwa wananchi wangu wa Jimbo la Mbogwe. Je, ni lini Serikali itaenda kutengeneza barabara hiyo?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu Mheshimiwa Fagason, Mbunge wa Jimbo la Mbogwe kwamba, tunafahamu sana umuhimu wa barabara hiyo na tayari Meneja wa TARURA Mkoa wa Geita na Wilaya ya Mbogwe tumeshawapa maelekezo wawasilishe gharama zinazohitajika kwa ajili ya kufanya marekebisho na matengenezo ya barabara hiyo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie kwamba, tunaendelea kuandaa utaratibu wa fedha na mara baada ya mvua hizi ambazo zimeendelea kunyesha kwa muda mrefu kupungua, Serikali itaanza kupeleka fedha kwa awamu kwa ajili ya ukarabati wa barabara hizo. Nimhakikishie tu hiyo barabara tutaipa kipaumbele. (Makofi
Name
Faraji Buriani Nandala
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ndanda
Primary Question
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:- Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?
Supplementary Question 3
MHE. FARAJI B. NANDALA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Hali ya barabara kwenye Jimbo la Ndanda ni changamoto kubwa sana, hasa Barabara kutoka Kata ya Mlingula, Kata ya Namajani, Kata ya Namatutwe kuelekea Kata ya Msikisi. Ni lini Serikali itaanza rasmi ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ziko barabara ambazo zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha changarawe, kiwango cha udongo na kiwango cha Barabara na Serikali hii imeweka mpango wa kuhakikisha tunahama kwenye ujenzi wa barabara za udongo kwenda zaidi kwenye changarawe, lakini pale panapowezekana kujenga barabara za lami.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, wakati wa utekelezaji wa mipango yetu ya ujenzi wa barabara tutaifanyia tathmini barabara hiyo na kuona uwezekano wa kupata fedha kwa ajili ya kuanza kujenga kwa awamu. Kwa changarawe ama kwa lami kwa kadri ambavyo fedha zitakuwa zimepatikana.
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Primary Question
MHE. DKT. GEORGE V. LUGOMELA aliuliza:- Je, lini Barabara kutoka Senani hadi Gula itakarabatiwa ili iweze kupitika wakati wa masika?
Supplementary Question 4
MHE. INNOCENT L. BASHUNGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya Chanyamisa – Bujara – Kihanga katika Kata ya Nyakasimbi imeharibika sana kutokana na mvua zinazoendelea, na Mheshimiwa Naibu Waziri anajua nimemfuata kuhusu hili. Je, ni lini barabara hii itapata fedha ili iweze kutengenezwa pamoja na barabara nyingine ambazo nimewasilisha kwake? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kaka yangu Mheshimiwa Innocent Lugha Bashungwa, Mbunge wa Jimbo la Karagwe amefuatilia mara kadhaa barabara hizi na amefika Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na ametuletea. Ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa namna ambavyo anawapambania wananchi wa Jimbo la Karagwe. Ninaomba nimhakikishie tu kwamba, tayari tumeshazipokea barabara zile na tunaendelea kuandaa utaratibu wa fedha ili kuanza ukarabati na ujenzi wa miundombinu muhimu katika barabara zile.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, ninaomba niwahakikishie wananchi wa Karagwe na Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali sikivu itakwenda kutekeleza miradi ya barabara hizo. ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved