Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 130 | 2026-04-20 |
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:-
Je, upi mkakati wa kurahisisha upatikanaji wa mikopo 10% kwa wanawake wa vijijini wanaokumbana na changamoto za mfumo wa mtandaoni?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kutatua changamoto za mfumo wa mtandao katika maombi ya mikopo ya 10% kwa makundi maalum yakiwemo ya wanawake wa vijijini, Serikali imechukua hatua zifuatazo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kuwawezesha waombaji kufanya usajili wa maombi ya ana kwa ana ambapo Maafisa Maendeleo ya Jamii kupitia Kamati za Kata za Huduma za Mikopo huvisaidia vikundi visivyokuwa na uwezo wa kutumia Mfumo wa kieletroniki wa WEZESHA katika kupata mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, Serikali imeendelea kuendesha mafunzo, ambapo katika Mwaka wa Fedha 2025/2026 shillingi bilioni 26.3 imetengwa kwa ajili ya usimamizi na ufuatiliaji, ikiwemo shillingi bilioni 7.9 ambapo jumla ya vikundi vya wanawake 24,064 vimefikiwa. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved