Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, upi mkakati wa kurahisisha upatikanaji wa mikopo 10% kwa wanawake wa vijijini wanaokumbana na changamoto za mfumo wa mtandaoni?
Supplementary Question 1
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali madogo mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; vikundi vingi vilivyopo vijijini katika Mkoa wa Mtwara vinajikita katika shughuli za kilimo, lakini moja ya kigezo ni kuonesha mashamba na wakati mwingine mazao hakuna. Je, Serikali haioni haja ya kuondoa hicho kigezo na kuzingatia uzalishaji ili wanawake hao waweze kupata mkopo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, vikundi vingi vimekuwa havikidhi vigezo hasa kwa kuwa hawana NIDA na hii ni katika maeneo mengi. Je, Serikali haioni haja, kwa kuwa hawa wananchi wanatambulika katika vijiji vyao, kupata barua kutoka kwa Serikali za Vijiji ili waweze kutambulika na kupata mikopo? (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninampongeza sana dada yangu na Katibu wetu Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum Mtwara. Kwa kweli amekuwa akichapa kazi sana kuwasemea wananchi wa Mkoa wa Mtwara na Watanzania kwa ujumla. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, nianze kwa kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tunafahamu kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo ya mikopo ya 10% kuna maelekezo ya namna ya kuhudumia mikopo hiyo na hasa muda wa kuanza kurejesha mikopo ya 10%. Muda wa kuanza kurejesha mikopo hiyo unategemea aina ya shughuli. Wapo akina mama ambao ni wakulima na mara nyingine wanakopa kwa ajili ya shughuli za kilimo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tutaendelea kuhakikisha kwamba tunawapa muda, kwa sababu tunafahamu kilimo uwekezaji wake unachukua muda mpaka baada ya kuanza kupata mazao ili kuanza kufanya marejesho. Katika jambo hilo tutaendelea kuhakikisha tunalisimamia ili wapate grace periods na baada ya hapo waanze kurejesha mara mazao yanapokuwa yamefika msimu wake wa mavuno.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, ni kweli kwamba ili upate mikopo hii kuna component ya NIDA, lakini Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alishatoa maelekezo kwamba, kama mwananchi hana NIDA lakini anafahamika katika eneo lake la kijiji au la kata, ana haki ya kupata mikopo hiyo. Kwa hiyo, ninaomba nitumie nafasi hii nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hili tumelichukua na tunalifanyia kazi ili kurahisisha mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana na wenye ulemavu. (Makofi)
Name
Samira Khalfan Amour
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza:- Je, upi mkakati wa kurahisisha upatikanaji wa mikopo 10% kwa wanawake wa vijijini wanaokumbana na changamoto za mfumo wa mtandaoni?
Supplementary Question 2
MHE. SAMIRA K. AMOUR: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itaweka utaratibu wa kuwafikia wanawake wa vijijini, Mkoani Kagera, kwa kupitia Maafisa Maendeleo ya Jamii ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo hiyo bila kikwazo cha mtandao? Ahsante, (Makofi)
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera na ninamhakikishia tu kwamba, Serikali inafahamu kwamba tuna maeneo ya vijijini na maeneo hayo mara nyingine vikundi hivi vinapata shida au ugumu wa kuwafikia Maafisa Maendeleo ya Jamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo ambalo limefanyika, moja ni kuhakikisha kwamba Maafisa Maendeleo ya Jamii wanafanya outreach Huduma Mkoba, kwa maana ya kwenda kwenye vijiji na kwenye kata kwa ajili ya kutoa elimu, kuhamasisha na kuviwezesha vikundi maalum kupata mikopo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la pili, tumeunda Kamati za Mikopo katika ngazi za kata na kamati hizi zinahusika kuwafikia wananchi katika vijiji. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tutaendelea kulisimamia hili, lakini tumelichukua kuongeza nguvu zaidi kwa Mkoa wa Kagera na mikoa mingine ili kuhakikisha kwamba vikundi hivi vinafikiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii na zile Kamati za Mikopo ili kutoa mikopo kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved