Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 131 | 2026-04-20 |
Name
Jesca David Kishoa
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko kubwa la Mazao ya Kilimo Wilaya ya Mkalama kama ilivyoahidi kwenye Ilani?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Jesca David Kishoa, Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa kujenga soko la mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama. Kwa kutambua umuhimu huo, tayari Halmashauri imepima na kupata hati miliki ya eneo la ujenzi wa soko lenye ukubwa wa ekari 7.2 katika Kata ya Nduguti ambapo ni Makao Makuu ya halmashauri na tathmini ya mazingira katika eneo hilo imefanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kazi inayoendelea ni kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa mradi huu ambao unatarajia kukamilika Juni, 2026. Baada ya upembuzi yakinifu kukamilika Serikali itatenga bajeti na kuanza ujenzi wa soko hilo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved