Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca David Kishoa
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko kubwa la Mazao ya Kilimo Wilaya ya Mkalama kama ilivyoahidi kwenye Ilani?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA D. KISHOA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Zaidi ya nusu mwaka sasa toka nyaraka zote muhimu kukabidhiwa kwenye mamlaka husika, ikiwepo barua, andiko la mradi, pamoja na environmental and social impact assessment, lakini mpaka sasa hakuna majibu yoyote. Swali la kwanza; wananchi wa Wilaya ya Mkalama wanataka kujua, barua na nyaraka zao zimekwamia wapi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; toka mwaka 2012 wilaya hii ilipoanzishwa, wakulima wanapoteza mapato yao 40% kwa sababu ya ukosefu wa soko. Ninaomba commitment ya Serikali, ni lini wanakwenda kujenga soko, ili wananchi wapate ajira, tuongeze pato la mtu mmoja mmoja pamoja na pato la halmashauri? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Jesca David Kishoa, Mbunge wa Iramba Mashariki, anawatendea haki sana wananchi wa Jimbo la Iramba Mashariki. Anawasemea kwa dhati kabisa, ameleta hoja hizi mara kadhaa na Serikali hii ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imezipokea kwa mikono miwili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, tunafahamu kuna uhitaji wa kujenga soko la mazao na ndiyo maana tayari timu ya wataalam ipo site tunavyoongea sasa na Juni au kabla ya Juni tutakuwa tumepata design yote, lakini na usanifu wa kina na baada ya hapo sasa tunatafuta fedha, kwa ajili ya ujenzi. Kwa hiyo, jambo la kwanza namhakikishia hakuna nyaraka ambayo haijafanyiwa kazi, nyaraka zote ambazo zimeletwa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, kutoka Mkalama zimefanyiwa kazi, ndiyo maana timu ipo pale site. Namhakikishia yeye na wananchi wa Mkalama kwamba, jambo hilo linakwenda kufanyika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili, tunafahamu kwamba, kuna upotevu wa mazao baada ya mavuno na wananchi wa Mkalama wanahitaji kupata soko, ili kuokoa mazao yanayopotea baada ya mavuno. Ninaomba nimhakikishie tu kwamba, tutakwenda kujenga soko hilo mapema iwezekanavyo baada ya fedha na usanifu huo kupatikana. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Agnesta Lambert Kaiza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA D. KISHOA aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Soko kubwa la Mazao ya Kilimo Wilaya ya Mkalama kama ilivyoahidi kwenye Ilani?
Supplementary Question 2
MHE. AGNESTA L. KAIZA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kuniona. Mheshimiwa Waziri, Kata ya Kisukuru yenye wakazi zaidi ya 50,000 haina soko, kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya wananchi wa Kata ya Kisukuru na haijawahi kabisa kuwa na soko na inasababisha wananchi hawa kwenda kutafuta mahitaji kwa kutembea umbali wa kilometa nne. Ninaomba kufahamu kauli ya Serikali, ni lini watajenga soko ndani ya Kata ya Kisukuru ili wananchi waweze kupata mahitaji yao? Ahsante.
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninampongeza sana Mheshimiwa Agnesta Lambert Kaiza, Mbunge wa Segerea, lakini ninaomba nitoe Kauli ya Serikali kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI kwamba, tumetoa maelekezo kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini, likiwemo Jiji la Ilala, kwamba, katika maeneo yote ambayo yanahitaji huduma muhimu kwa wananchi, kama masoko, katika mipango yao ya kila mwaka ya mapato ya ndani lazima waweke kipaumbele.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jiji la Dar es Salaam ni moja ya majiji ambayo yana mapato makubwa zaidi katika nchi yetu. Kwa hiyo, ninatumia nafasi hii kumwelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam kwamba, wafanye tathmini eneo la Kata ya Kisukuru waone uwezekano wa kuanza kutenga fedha kwa awamu, kwa ajili ya kujenga soko kwa sababu, ni huduma za jamii, lakini pia, ni chanzo cha mapato kwa Jiji la Dar es Salaam. Ahsante sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved