Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 132 2026-04-20

Name

Azza Hilal Hamad

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AZZA H. HAMAD aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kuunganisha Barabara ya lami ya Kahama – Njiapanda ya Lohumbo, Mji Mdogo wa Didia?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Azza Hillal Hamad, Mbunge wa Jimbo la Itwangi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Didia – Solwa yenye urefu wa kilometa 55.3 inayounganisha Majimbo ya Itwangi na Solwa imekuwa ikitengewa fedha na Serikali, kwa ajili ya ukarabati. Katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imetumia shilingi milioni 131.78 kuchonga kilometa 14, kuweka changarawe na ujenzi wa makalavati matatu. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, jumla shilingi milioni 318.94 zilitumika, kwa ajili ya kuchonga na kuweka changarawe kilometa 13, pamoja na ujenzi wa makalavati manne.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kipande cha barabara kinachoombewa kuwekwa lami kina urefu wa kilometa 4.5 kikiwa ni sehemu ya Barabara ya Didia – Solwa inayoanzia katika Barabara ya Tinde – Isaka – Ushirombo. Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini umeweka katika mipango yake ya mwaka wa fedha 2026/2027 kufanya usanifu, kwa ajili ya kipande hiki cha barabara kwa lengo la kujua gharama halisi za utekelezaji wa ujenzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mara baada kujua gharama halisi, Serikali itaweka kwenye mipango ya fedha, kwa ajili ya kutekeleza ujenzi kwa tabaka la lami kipande cha Barabara ya Njiapanda ya Lohumbo, Mji Mdogo wa Didia, kilomEta 4.5. Ahsante.