Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 136 | 2026-04-20 |
Name
Haiderali Hussein Gulamali
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ilongero
Primary Question
MHE. YOHANA S. MSITA K.n.y. MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA Ilongero?
Name
Wanu Hafidh Ameir
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali Namba 136 la Mheshimiwa Haiderali Hussein Gulamali, Mbunge wa Ilongero, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA) 65 katika Wilaya Sitini na Nne (64) na Mkoa mmoja (01) wa Songwe. Ujenzi huu unafanyika katika Wilaya au Mkoa ambao hauna Chuo cha VETA kabisa. Jimbo la Ilongero lipo katika Wilaya ya Singida ambapo tayari ina Chuo cha VETA. Hivyo, wananchi wa Jimbo la Ilongero wanahimizwa kutumia Chuo cha VETA Singida ambacho kina huduma za bweni kwa wanafunzi wanaotoka maeneo ya mbali.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kupanua fursa za upatikanaji na elimu ujuzi kwa ngazi mbalimbali, Serikali inaendelea na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Amali katika Jimbo la Ilongero ambayo itatoa mafunzo ya vitendo na stadi zinazohitajika katika soko la ajira.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved