Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yohana Stephen Msita

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Itigi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA K.n.y. MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA Ilongero?

Supplementary Question 1

MHE. YOHANA S. MSITA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina swali moja la nyongeza. kwa kuwa Wilaya ya Manyoni ni miongoni mwa Wilaya kubwa sana hasa kwenye Mkoa wa Singida, ina zaidi ya 58%. Tunaishukuru sana Serikali kwa sababu imeshaanza ujenzi wa VETA, lakini ujenzi huu umekuwa ukisuasua. Je, ni lini Chuo cha VETA Wilaya ya Manyoni kitakamilika ili kiweze kuanza kazi? (Makofi)

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yohana Msita wa Jimbo la Itigi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivi sasa ujenzi wa VETA kwa ujumla umefikia 65% na Serikali kama ilivyoahidi kwamba itajenga vyuo hivi vya VETA nchini nzima kama ilivyoahidi, tunaahidi kwamba 35% iliyobaki ikifika mwezi Septemba mwaka 2026 itakuwa imemalizika. (Makofi)

Name

Thomas Maganga Kampala

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Katavi

Primary Question

MHE. YOHANA S. MSITA K.n.y. MHE. HAIDERALI H. GULAMALI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza ahadi ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi VETA Ilongero?

Supplementary Question 2

MHE. ENG. AMOSY W. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mkataba wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Wilayani Sikonge ulisainiwa Juni, 2023 na chuo kingekamilika Disemba, 2023, lakini kutokana na changamoto mbalimbali mpaka tunavyoongea hivi sasa hicho chuo bado hakijakamilika. Je, ni nini sasa tamko la Serikali kuona kwamba chuo hiki kinaenda kukamilika? (Makofi)

Name

Wanu Hafidh Ameir

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu katika majibu ya jumla kwamba Serikali iliahidi kujenga vyuo hivi nchi nzima kwa zile Wilaya ambazo hazina vyuo hivi. Tayari tulishapokea shilingi bilioni 82 kama 82% ya shilingi bilioni mia moja ambazo tumepewa, lakini pia tumeshapokea asilimia ya fedha zilizobakia na nimuahidi Mbunge kwamba fedha hizi tutaenda kuzigawa hivi karibuni na vyuo vyote hivi vitakamilika. (Makofi)