Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo | 137 | 2026-04-20 |
Name
Mariam Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. STELLA I. ALEX K.n.y. MHE. MARIAM N. KISANGI aliuliza:-
Je, wananchi wa Temeke wananufaikaje na uwepo wa Uwanja wa Taifa uliopo Wilayani humo?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA, NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Uwanja wa Benjamin Mkapa una faida nyingi kwa wananchi wa Manispaa ya Temeke na Taifa kwa ujumla. Kiuchumi unachochea mzunguko wa fedha kwa wafanyabiashara wakati wa matukio makubwa, pia unavutia wawekezaji wa matangazo makubwa na ajira kwa wananchi. Kijamii, matukio makubwa ya kidini na matamasha makubwa ya sanaa na muziki yanawaleta Wanatemeke na Watanzania wote pamoja na hivyo kudumisha amani na mshikamano wa nchi yetu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kimichezo uwepo wa uwanja huu umeifanya Manispaa ya Temeke kuwa kitovu cha michezo ya kitaifa na kimataifa jambo linaloongeza heshima na utambulisho wa eneo hilo na kutoa hamasa kwa vijana kushiriki michezo. Hivyo, miundombinu hii ni muhimu katika kuchochea maendeleo kwa wananchi wa Temeke na Tanzania kwa ujumla.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved