Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 12 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 138 2026-04-20

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: -

Je, lini mnara wa Redio Tanzania uliojengwa Kiteto utaanza kufanya kazi?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo hiki ni sehemu ya mradi unaotekelezwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kushirikiana na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF). Hadi kufikia tarehe 14 Aprili, 2026 ujenzi na ufungaji wa miundombinu ya mitambo ya redio katika kituo hiki umefikia 90% na unatarajiwa kukamilika ifikapo Juni, 2026. Ninakushukuru.