Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Edward Olelekaita Kisau

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kiteto

Primary Question

MHE. EDWARD O. KISAU aliuliza: - Je, lini mnara wa Redio Tanzania uliojengwa Kiteto utaanza kufanya kazi?

Supplementary Question 1

MHE. EDWARD O. KISAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Niipongeze Serikali kwa majibu mazuri, mafupi, safi. Sasa swali dogo tu la nyongeza. Kwa siku ambazo si nyingi sana ni lini upo tayari ututembelee Kiteto ili kuweza ku-monitor mradi huu muhimu sana kwa wananchi wa Kiteto?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nishukuru kwa zuri la nyongeza la Mheshimiwa Olelekaita, Mbunge wa Kiteto na nimpongeze kwa kazi kubwa anayoifanya kuwapigania Wanakiteto. Hili la kuambatana naye kwenda Kiteto wala siyo suala la mjadala, atakapokuwa tayari Mheshimiwa Mbunge anifahamishe tujadiliane kuhusiana na ratiba ya Bunge na shughuli nyingine za Serikali, tufunge safari kwa ajili ya kwenda Kiteto.