Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 141 | 2026-04-20 |
Name
Dr. Yahaya Esmail Nawanda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. DKT. YAHYA E. NAWANDA aliuliza:-
Je, lini Mradi wa Maji wa Makonde utakamilika?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Esmail Nawanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Makonde kupitia Mradi wa Maji wa Miji 28 kwa gharama ya shilingi bilioni 84.7. Kazi zinazotekelezwa katika mradi huo ni pamoja na uchimbaji wa visima virefu vitatu vyenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 26 kwa siku, ujenzi wa matanki manne yenye jumla ya ujazo wa lita milioni 13, sanjari na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 70.
Mheshimiwa Mwenyekiti, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa 40%, ambapo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba, 2026 na kunufaisha zaidi ya wananchi 600,000 waishio kwenye Wilaya za Newala, Tandahimba pamoja na Mji wa Nyanyamba.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved