Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 12 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 143 | 2026-04-20 |
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kasindaga – Kyebitembe – Karambi hadi Runazi kwa kiwango cha lami?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Oscar Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Kasindaga hadi Runazi yenye urefu wa kilometa 37.6 ni barabara ya mkoa, inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Kagera. Kwa sasa, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Baada ya usanifu kukamilika na gharama za ujenzi kujulikana, Serikali itatafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved