Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO aliuliza:- Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Kasindaga – Kyebitembe – Karambi hadi Runazi kwa kiwango cha lami?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Mwenyekiti ninashukuru sana kwa kunipa fursa ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kwa kuwa hii barabara ambayo inahudumiwa na TANROADS kutokana na mvua zinazoendelea imeharibika sana kiasi kwamba haiwezi kuhudumia wananchi wa maeneo hayo; je, Serikali ina mkakati gani wa kuikarabati kwa kipindi hiki ili iendelee kutoa huduma kwa wananchi?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; barabara hii inahudumia Tarafa ya Kimwani ambayo ina wakazi wengi wa Wilaya ya Muleba na ndiyo inabeba uchumi wa Wilaya ya Muleba. Je, Serikali haioni uharaka wa kutafuta hizo pesa tukaifanyia upembuzi wa kina ili ikajengwe kwa kiwango cha lami? (Makofi)
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nikubaliane na Mheshimiwa Mbunge kwamba, barabara nyingi ambazo ni za kiwango cha changarawe katika kipindi hiki cha mvua zimeharibika ikiwepo na hii barabara ambayo nimeisema. Hata hivyo, nimwelekeze tu Meneja wa Mkoa wa Kagera kwamba, waweze kufanya kinachowezekana pale ambapo panaweza pakafanyika, basi mkandarasi ambaye amepewa kazi ya kukarabati hiyo barabara aweze kuwepo kwenye hiyo barabara ili yale maeneo yote ambayo wananchi wanakwama aweze kuyarekebisha ili barabara iweze kupitika.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali lake la pili, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Mkoa wa Kagera kwa maana ya Meneja wa Mkoa, wameshawasilisha maombi ya kuiweka barabara hii kwenye usanifu katika bajeti ambayo kama itapita, basi nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge hilo zoezi la kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, litakuwa ni kazi ambayo tutaifanya katika mwaka wa fedha ambao tutauanza Julai. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved