Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 32 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 372 | 2026-05-19 |
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga zahanati Kijiji cha Zugumlole itakayohudumia Vitongoji vya Kaung’ando, Ibasa “A” na “B”, Mkombozi, Ulinda na Ndevelwa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Kijiji cha Zugumlole kipo katika Kata ya Ndevelwa, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora. Kijiji hicho kina jumla ya wakazi 1,989, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. Kwa sasa wananchi wa Kijiji cha Zugumlole wanapata huduma katika Zahanati ya Ndevelwa iliyopo kilometa 25 kutoka kijijini hapo. Aidha, kwa upande wa huduma za upasuaji wanahudumiwa kwenye Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Tabora iliyopo kilometa 42.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutoka na umuhimu wa kuwepo kwa zahanati katika Kijiji cha Zugumlole, Serikali ya Wilaya ya Tabora ilifika na kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Zugumlole na kuhamasisha wananchi ili waanze ujenzi wa boma la zahanati na Serikali itatoa fedha za kukamilisha boma kadri utaratibu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi kote nchini kwa awamu. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved