Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 32 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 374 | 2026-05-19 |
Name
Dickson Nathan Lutevele
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafinga Mjini
Primary Question
MHE. DICKSON N. LUTEVELE aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga stand ya kisasa ya mabasi Halmashauri ya Mji wa Mafinga?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dickson Nathan Lutevele Villa, Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ina mapango wa kujenga stand ya kisasa ya mabasi katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga katika Kata ya Kinyanambo kupitia Mradi wa Kuboresha Miundombinu ya Miji (TACTIC) Awamu ya Tatu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifu na usanifu wa awali ulikamilika mwezi Februari, 2026 na taarifa ilishawasilishwa kwa timu ya uratibu wa miradi ya Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI na Halmashauri ya Mji wa Mafinga. Kwa sasa Mtaalam Mshauri Kampuni ya Botek Bosphorus Consulting Corporation kwa kushirikiana na kampuni ya Building design Authority (P) Ltd wanaendelea kufanya usanifu wa mwisho ambao unatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2026.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya usanifu kukamilika, hatua itakayofuata ni kutangaza zabuni kwa ajili ya kupata mkandarasi mjenzi. Pindi taratibu hizo zikikamilika, ujenzi wa stand ya mabasi katika mji wa Mafinga utaanza mara moja. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved