Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 32 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 375 | 2026-05-19 |
Name
Tarimba Gulam Abbas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kinondoni
Primary Question
MHE. TARIMBA G. ABBAS aliuliza: -
Je, kuna mpango gani wa kuondoa mgongano wa Vikao vya Bunge na Halmashauri za Majiji, Manispaa na Miji ili Wabunge washiriki?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Tarimba Gulam Abbas, Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwenye nyakati tofauti, imekuwa ikitoa maelekezo kwa halmashauri ili kuhakikisha kwa kiwango kikubwa, ratiba za vikao vya halmashauri hazigongani na ratiba za Vikao vya Bunge. Halmashauri zilielekezwa kuzingatia kalenda ya shughuli za Bunge wakati wa kuandaa kalenda zao za vikao vya mwaka husika ili kutoa fursa kwa Wabunge ambao ni wajumbe wa mikutano hiyo, kushiriki kikamilifu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, itaendelea kuzisimamia halmashauri kuhakikisha zinaandaa ratiba ya vikao kwa mwaka 2026/2027 kwa kuzingatia ratiba za vikao vya Bunge kwa kadri itakavyowezekana. Aidha, Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, wanaelekezwa kuwasiliana na Waheshimiwa Wabunge wakati wa kupanga ratiba za Vikao vya Kamati na Mabaraza ya Madiwani, ili kuona namna viongozi hao wanaweza kushiriki katika vikao hivyo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved