Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 32 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Rais: Maendeleo ya Vijana 376 2026-05-19

Name

Latifa Khamis Juwakali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje katika kutafuta fursa za kuwawezesha vijana?

Name

Joel Arthur Nanauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mtwara Mjini

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MAENDELEO YA VIJANA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Latifa Khamis Juwakali, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuongeza fursa za uwezeshaji wa vijana ikiwemo ajira na kujiajiri, kupitia miradi ya maendeleo, uboreshaji wa mazingira ya biashara na uwekezaji, na kuondoa vikwazo mbalimbali vya kimfumo. Miongoni mwa hatua zinazotekelezwa ni uratibu wa programu za uwezeshaji vijana kupitia Wizara za Kisekta kama vile Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Madini, Viwanda na Biashara, Sanaa na Michezo, Teknolojia ya Habari na nyinginezo, sambamba na utoaji wa mikopo yenye masharti nafuu kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana, asilimia nne ya mapato ya halmashauri na asilimia kumi ya zabuni za umma kwa vijana kupitia Public Procurement Regulatory Authority (PPRA). Hatua ambazo zimeendelea kuongeza upatikanaji wa mitaji, ajira na fursa za kiuchumi kwa vijana nchini. Aidha, Serikali imeendelea kutafuta na kuratibu fursa za vijana za ajira ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuongeza ushiriki wa vijana katika shughuli za kiuchumi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.